Tuesday, January 1, 2008

Mwana FA



Pichani ni Hamisi Mwinjuma aka Mwanafalsafa(MwanaFA).Msanii huyu wa muziki wa kizazi kipya ni miongoni mwa wasanii ambao wanasifika sana kwa kuwa na mashairi makali na yenye ujumbe mzito nchini Tanzania.Pengine yeye mwenyewe alilijua hilo wakati anaingia kwenye fani ya muziki na ndio maana akaamua kujiita Mwanafalsafa.Hatujui,siku moja tutamuuliza.

Mwanafalsafa ameshatunga mashairi na nyimbo nyingi.Miongoni mwa nyimbo au mashairi hayo ni lile ambalo inasemekana ndio “lilimtoa”.Aliliita “Ingekuwa Vipi”.Humo alikuwa anahoji mambo kadhaa kama vile;

Ingekuwa vipi Yesu angerudi?Angemaliza vita ya Wapalestina na Wayahudi? lngekuwa vipi kama Osama angeutawala Ulimwengu?Wamarekani Uarabuni wangekuwa Sungusungu?Ungekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini?Dunia bila dhambi,Kipimo cha uovu nini?Polisi, mahakama na gerezani angeenda nani?Vipi kama Wazungu wasingeingia Afrika? Magari, ndege, Reli na nguo, nani angeleta?Na bila biashara ya utumwa wangekuwepo black Americans? …na mengineyo.

Unaweza kuusikiliza wimbo huo wa MwanaFA kupitia EastafricanTube kwa kubonyeza hapa.

1 comment:

Jeff Msangi said...
This comment has been removed by the author.