Monday, March 17, 2008

Misifa Uscandinavia!



Kama kawaida yake ni yuleyuleee mzee wa Misifa a.k.a Dully Sykes kama anavyojulikana kwasana washabiki wake...na habari zilizoifikia meza yetu ni kwamba kijana huyu mtoto wa ilala,hivi karibuni atapiga tour la kujisha katika nchi za Scandinavia.
Taarifa kutoka ndani ya kambi ya msanii huyo,ilisema kuwa Dully katika ziara hiyo anatarajia kwenda nchi za Denmark,Norway na Finland...ambapo kwasasa yuko chimbo kujiandaa vyema kwa ziara hiyo ambayo kwa hakika itakuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wabongo waishio ktk nchi zilizotajwa hapo juu.

Ziara hili limekuja baada mafanikio ya ziara yake ya mwaka jana nchini Uholanzi.

Haya kaka mungu akupe nini....nenda kafanye kweli...sio ukalete misifa tena huko!

JITA RECORD'S SASA YAWA TISHIO DAR


Jita Record's sasa inazidi umiza vichwa baadhi ya wa miliki wa studio kutokana na ubora wa kazi zinazo fanyika hapo pia producer XG a.k.a GOD nyani anazidi umiza pia vichwa vya ma producer wengine baada ya kukamirisha kazi ya msanii mahiri wa mziki wa Hiphop Mansuli