Friday, April 4, 2008

Moto kuwaka BSS leo!


Patakuwa hapatoshi leo kwenye ukumbi uliopo ndani hoteli ya Blue Pearl ndani ya jengo la Ubungo Plaza ambapo wakali wa 5 watatupa karata zao za mwisho katika fainali za kutafuta mshindi wa shindano la kutafuta vipaji la Bongo Star Search (BSS) atakayesunda kwapani kitita cha Dola 15,000 na ofa ya kurekodi video ya kwanza katika kampuni ya Benchmark Production.

Sambamba na fainali hizo kunatazamiwa kuwa na makamuzi ya kufa mtu kutoka kwa kina dada wakali wa Kijamaica 'Brick & Lace', wanaotamba na wimbo wao wa 'Love is Wicked'.
Fainali hiyo, inatazamiwa kuwa ya `vuta nikuvute`kutokana na washiriki hao....Roger Lucas, Maangaza Nyange, Misoji Edward, Yohanna Simon na Elynema Mbwambo kuwa na vipaji tofauti tofauti visivyotabirika.

Yohana na sauti yake nzito atakuwa akisubiriwa kwa hamu ili kuona atarusha karata yake kwa kutumia staili ipi.

Ameonekana kumudu fani mbalimbali kutokana na sauti yake maridadi.

Misoji Nkwabi, ambaye amweza kuteka watu kutokana na uwezo wake wa kuimba nyimbo za wasanii wa Afrika Kusini kama marehemu Brenda Fassie na nyakati fulani hata nyimbo za wasanii wa Ulaya.

Hata hivyo, makali yake zaidi yamekuwa katika muziki wa Injili, ambao umetoka kuwa na mashabiki wengi.

Bila ya shaka yoyote kura zake nyingi atazipata kutoka kwa wapenzi wa muziki wa Injili.

Rogers Lucas, `mtaalamu` wa kutunga nyimbo zake mwenye, kipaji ambacho ni cha nadra sana.

Rogers na gitaa lake pengine ataibuka na wimbo wa kuweza kuzingua watu watakaokuwa wanashuhudia shoo ya leo.

Elynema, aliyefurahi mno na kuparamia nguzo ukumbini, Jumapili iliyopita baada ya kuingia tano bora, ana nafasi nzuri ya kuweza kufanya vizuri kutokana sauti yake kuwa ya kuvutia.

Mashabiki wa taarabu watakuwa `beneti` na Maangaza, ambaye toka mwanzo wa shindano hilo amekuwa aking`ara kutokana na kuimba nyimbo za taarab.

Pia kuna habari tayari makundi mbalimbali ya taarab yanamnyemelea mshiriki huyo.

Ili kupata mshindi, majaji wana asilimia 60 kwenye maamuzi ya kura za kuamua.Asilimia 40 ni kura zitazopigwa na mashabiki watakaoshuhudia fainali hiyo kupitia kituo cha televisheni cha ITV kitakachorusha fainali hiyo moja kwa moja.

Pamoja na Brick & Lace, wengine watakaotoa burundani leo ni pamoja na mshindi wa mwaka jana wa BSS, Jumanne Iddi, Aboubakary Mzuri, Kala Jeremiah na Mrisho Rajabu.

Kiingilio kitakuwa sh. 35,000 kwa viti maalum na sh. 20,000 kwa sehemu za kawaida.

Wadhamini wa shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, Coca Cola, LG, Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS), The Living Room, hoteli ya Giraffe Ocean View, GMC, Mariedo, Sadolin, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Kilimanjaro Drinking Water.

BSS wakamatishwa Bingo zao!



Mshindi wa (BSS) Bongo Star Search 2008,mwanadada Misoji Mkwabi jana alikamatishwa rasmi zawadi zake za ushindi kutoka kwa wadhamimi wa shindano hilo.

Mbali na mwanadada huyo wengine waliokabidhiwa zawadi zao...ni wale washiriki wengine waliobahatika kufikia hatua ya top 10.

Zawadi zilizotolewa kwa mshindi wa kwanza ni hundi ya dola za kimarekani 15,000,Television inchi 29 kutoka Kampuni ya LG, simu ya mkononi, fulana, kutoka kampuni hiyo hiyo, seti ya Sofa, kutoka Kampuni ya Living Room, Computer....pamoja na kurekodi albamu katika studio ya GMC.
Mbali na zawadi hiyo pia Misoji alikabidhiwa zawadi ya Sh. milioni 1 taslimu kutoka (FHI) Family Health Internation, kwa ajili ya kutunga nyimbo bora ya Ukimwi.

Mshindi wa pili katika shindano hilo, ambaye ni Rogers Lucas alizawadiwa Fridge,Simu ya mkononi, kutoka Kampuni ya LG,Computer....Sh. 500,000 kutoka Benchmark, pamoja na zawadi ya nguo kutoka kwa moja ya wadhamini Mariedo Botique na Sh. 150,000 kutoka FHI kwa ajili ya kutunga nyimbo ya Ukimwi.

Mshindi wa tatu katika shindano hilo, ambaye ni Elynema Mbwambo alizawadiwa DVD player, simu ya mkononi, kutoka Kampuni ya LG, Komputa kutoka Desktop, Sh. 500,000, kutoka Benchmark, nguo kutoka Mariedo Botique, pamoja na hundi ya Sh. 500,000 kutoka Shear Illusion.

Wakati mshindi wa nne katika shindano hilo ni Yohana Simon, aliyezawadiwa pesa taslimu Sh. 500,000 kutoka Benchmark, Min Stereo, simu ya mkononi kutoka LG, komputa kutoka Desk top, pamoja na mavazi kutoka kwa Mariedo Botique.

Maangaza Nyange ambae alikuwa mshindi wa tano katika shindano hilo, alizawadiwa Sh. 500,000 kutoka Benchmark, Computer, kutoka Desktop,simu ya mkononi, kutoka LG, pamoja na mavazi kutoka Mariedo Botique, pamoja na sh 600,000 kwa ajili ya kuwa mshindi wa pili wa kutunga nyimbo inayohusu ukimwi.

Washiriki wengine waliongia katika 10, bora walipata kifuta jasho cha sh 500,000 kutoka Benchmark, pamoja na simu za mkononi kutoka Kampuni ya LG.