Friday, April 4, 2008

Moto kuwaka BSS leo!


Patakuwa hapatoshi leo kwenye ukumbi uliopo ndani hoteli ya Blue Pearl ndani ya jengo la Ubungo Plaza ambapo wakali wa 5 watatupa karata zao za mwisho katika fainali za kutafuta mshindi wa shindano la kutafuta vipaji la Bongo Star Search (BSS) atakayesunda kwapani kitita cha Dola 15,000 na ofa ya kurekodi video ya kwanza katika kampuni ya Benchmark Production.

Sambamba na fainali hizo kunatazamiwa kuwa na makamuzi ya kufa mtu kutoka kwa kina dada wakali wa Kijamaica 'Brick & Lace', wanaotamba na wimbo wao wa 'Love is Wicked'.
Fainali hiyo, inatazamiwa kuwa ya `vuta nikuvute`kutokana na washiriki hao....Roger Lucas, Maangaza Nyange, Misoji Edward, Yohanna Simon na Elynema Mbwambo kuwa na vipaji tofauti tofauti visivyotabirika.

Yohana na sauti yake nzito atakuwa akisubiriwa kwa hamu ili kuona atarusha karata yake kwa kutumia staili ipi.

Ameonekana kumudu fani mbalimbali kutokana na sauti yake maridadi.

Misoji Nkwabi, ambaye amweza kuteka watu kutokana na uwezo wake wa kuimba nyimbo za wasanii wa Afrika Kusini kama marehemu Brenda Fassie na nyakati fulani hata nyimbo za wasanii wa Ulaya.

Hata hivyo, makali yake zaidi yamekuwa katika muziki wa Injili, ambao umetoka kuwa na mashabiki wengi.

Bila ya shaka yoyote kura zake nyingi atazipata kutoka kwa wapenzi wa muziki wa Injili.

Rogers Lucas, `mtaalamu` wa kutunga nyimbo zake mwenye, kipaji ambacho ni cha nadra sana.

Rogers na gitaa lake pengine ataibuka na wimbo wa kuweza kuzingua watu watakaokuwa wanashuhudia shoo ya leo.

Elynema, aliyefurahi mno na kuparamia nguzo ukumbini, Jumapili iliyopita baada ya kuingia tano bora, ana nafasi nzuri ya kuweza kufanya vizuri kutokana sauti yake kuwa ya kuvutia.

Mashabiki wa taarabu watakuwa `beneti` na Maangaza, ambaye toka mwanzo wa shindano hilo amekuwa aking`ara kutokana na kuimba nyimbo za taarab.

Pia kuna habari tayari makundi mbalimbali ya taarab yanamnyemelea mshiriki huyo.

Ili kupata mshindi, majaji wana asilimia 60 kwenye maamuzi ya kura za kuamua.Asilimia 40 ni kura zitazopigwa na mashabiki watakaoshuhudia fainali hiyo kupitia kituo cha televisheni cha ITV kitakachorusha fainali hiyo moja kwa moja.

Pamoja na Brick & Lace, wengine watakaotoa burundani leo ni pamoja na mshindi wa mwaka jana wa BSS, Jumanne Iddi, Aboubakary Mzuri, Kala Jeremiah na Mrisho Rajabu.

Kiingilio kitakuwa sh. 35,000 kwa viti maalum na sh. 20,000 kwa sehemu za kawaida.

Wadhamini wa shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, Coca Cola, LG, Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS), The Living Room, hoteli ya Giraffe Ocean View, GMC, Mariedo, Sadolin, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Kilimanjaro Drinking Water.

BSS wakamatishwa Bingo zao!Mshindi wa (BSS) Bongo Star Search 2008,mwanadada Misoji Mkwabi jana alikamatishwa rasmi zawadi zake za ushindi kutoka kwa wadhamimi wa shindano hilo.

Mbali na mwanadada huyo wengine waliokabidhiwa zawadi zao...ni wale washiriki wengine waliobahatika kufikia hatua ya top 10.

Zawadi zilizotolewa kwa mshindi wa kwanza ni hundi ya dola za kimarekani 15,000,Television inchi 29 kutoka Kampuni ya LG, simu ya mkononi, fulana, kutoka kampuni hiyo hiyo, seti ya Sofa, kutoka Kampuni ya Living Room, Computer....pamoja na kurekodi albamu katika studio ya GMC.
Mbali na zawadi hiyo pia Misoji alikabidhiwa zawadi ya Sh. milioni 1 taslimu kutoka (FHI) Family Health Internation, kwa ajili ya kutunga nyimbo bora ya Ukimwi.

Mshindi wa pili katika shindano hilo, ambaye ni Rogers Lucas alizawadiwa Fridge,Simu ya mkononi, kutoka Kampuni ya LG,Computer....Sh. 500,000 kutoka Benchmark, pamoja na zawadi ya nguo kutoka kwa moja ya wadhamini Mariedo Botique na Sh. 150,000 kutoka FHI kwa ajili ya kutunga nyimbo ya Ukimwi.

Mshindi wa tatu katika shindano hilo, ambaye ni Elynema Mbwambo alizawadiwa DVD player, simu ya mkononi, kutoka Kampuni ya LG, Komputa kutoka Desktop, Sh. 500,000, kutoka Benchmark, nguo kutoka Mariedo Botique, pamoja na hundi ya Sh. 500,000 kutoka Shear Illusion.

Wakati mshindi wa nne katika shindano hilo ni Yohana Simon, aliyezawadiwa pesa taslimu Sh. 500,000 kutoka Benchmark, Min Stereo, simu ya mkononi kutoka LG, komputa kutoka Desk top, pamoja na mavazi kutoka kwa Mariedo Botique.

Maangaza Nyange ambae alikuwa mshindi wa tano katika shindano hilo, alizawadiwa Sh. 500,000 kutoka Benchmark, Computer, kutoka Desktop,simu ya mkononi, kutoka LG, pamoja na mavazi kutoka Mariedo Botique, pamoja na sh 600,000 kwa ajili ya kuwa mshindi wa pili wa kutunga nyimbo inayohusu ukimwi.

Washiriki wengine waliongia katika 10, bora walipata kifuta jasho cha sh 500,000 kutoka Benchmark, pamoja na simu za mkononi kutoka Kampuni ya LG.

Sunday, March 23, 2008

XG (GOD NYANI) PRODUCER WA JITA RECORDS


Huyu ndiye producer XG anaye fanya maproducer wakongwe wa dar waumize vichwa pia wasanii ma superstars kama Sqeezer na Mansoor kumkubali
Ebwana hapa akitafuta sample kiaina chemba

Tuesday, March 18, 2008

Muungano nje ya Tip Top!Katika hali ambayo naweza kuiita ya kushangaza...wale wasanii wawili maswahiba......Mb Dogg na mwenzake Deso, ambao sio siku nyingi zilizopita walijitoa kwenye kundi lao la zamani la...'Tip Top Connection' wameungana na kuunda umoja wao Chini ya jina la 'Wamanza Bay'.
Kwa mujibu wa wawili hao....lengo la muungano huo ni kusaidiana katika kazi zao za sanaa kama familia na wala sio kama kundi.

``Tumekuwa na mahusiano mazuri tangu tukiwa ndani ya kundi letu la zamani....tumeona iko haja ya kukaa pamoja na kushirikiana.....ni ushirikiano wa kupeana kampani katika mambo mengi ya kikazi,`` alisema Deso.

``Kila msanii anaweza kuendelea kufanya kazi zake kivyake na kutoa albam zake lakini, unafanya hivyo huku ukijua una mtu ama watu wa familia yako wanaokusapoti.....ndio maana nzima ya familia yetu hii,`` alisema Deso.

Hivi sasa kundi hilo linajiandaa kupiga picha za pamoja kwa ajili ya kuutangaza muunganiko wao...na wana imani mambo yakienda kama yalivyopangwa watafanya familia kubwa zaidi na kuibua vipaji vya wasanii wengi waliofichika.

Tuzo za vinara wa Filamu kusheheni Mei 2008Baada ya kufana kwa uzinduzi wa Tuzo za Vinara wa filamu Tanzania, na waandaaji wanaalikwa kujaza fomu za ushiriki ili kuweza kuwasilisha kazi zao katika Tuzo za 2008.
Fomu hizi zitapatikana ndani ya ofisi za BASATA (Muulizie Omar Mayanga), Wananchi Wote, Kapico, GMC na Game First Quality.

Baada ya kujaza fomu watengezaji wa filamu wanatakiwa kurudisha fomu na nakala ya kazi kwenye ofisi za BASATA kwa Omar Mayanga.

Pia utoaji tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania unalenga katika kuifanya sanaa ya Tanzania kupata nguvu mpya na kuwafanya watengenezaji na wadau wa sanaa kufanya bidii katika ushindani wa soko la sanaa.

Wameamua kufanya hivyo ili kutengeneza kazi zilizo bora zaidi zinazoweza kuuzika kimataifa, ili nchi yetu iwe katika ramani ya dunia.

Tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania pia zinalenga kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na mwamko wa kupenda kaz, zinazotengenezwa na Watanzania wenzao ili kupata mafunzo mbalimbali yatokanayo na kazi za wasanii na pia kukuza soko kwa faida ya pande zote mbili.

Katika fomu hizo, kutaainishwa mambo muhimu ambayo mtengenezaji wa filamu atapaswa kujaza.

Fomu hiyo itakuwa na maswali mengine yaani filamu imetengenezwa lini, mahali ilikotengenezwa, maudhui ya filamu na lugha iliyotumika.

Baada ya fomu hizo kujazwa kwa usahihi, zitatumwa kwenye ofisi za waandaji, kwa mkono au njia ya posta kwa anuani kamili ya waandaji. Watengenezaji wa filamu husika watapaswa kuambatanisha na mkanda wa filamu (VHS/DVD/VCD).

Kutakuwa na jopo la majaji wanane (8) watakaochaguliwa na waandaji kwa kushirikiana na Baraza la sanaa la Taifa nchini, watakaokuwa na jukumu la kupitia filamu zote na kuzitolea uamuzi.

Majina na wasifu za majaji zitawekwa bayana hivi karibuni, pia vigezo zitakazotumika zitawekwa wazi.

Filamu zitakazoingizwa kuwania tuzo ni zile zilizotengenezwa na Watanzania kuanzia Januari 2007 hadi mwisho wa siku ya kualikwa watengenezaji kuingiza filamu zao ambayo itakuwa 31 Machi 2008.

Kushiriki kwa watengezaji wa filamu itasaidia kupata Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Mwongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu, Mtunzi Bora wa Filamu, Filamu Bora ya kutisha, Muigizaji Mwandamizii Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike; Adui Bora kwenye Filamu, Mhariri Bora wa Filamu na mapambo na maleba ya mwaka.

Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa machango wao kukuza sanaa ya hapa nchini.

Tukio la utoaji wa tuzo hizi limepangwa kufanyika mwezi Mei 2008 na litafanyika kila mwaka.

Monday, March 17, 2008

Misifa Uscandinavia!Kama kawaida yake ni yuleyuleee mzee wa Misifa a.k.a Dully Sykes kama anavyojulikana kwasana washabiki wake...na habari zilizoifikia meza yetu ni kwamba kijana huyu mtoto wa ilala,hivi karibuni atapiga tour la kujisha katika nchi za Scandinavia.
Taarifa kutoka ndani ya kambi ya msanii huyo,ilisema kuwa Dully katika ziara hiyo anatarajia kwenda nchi za Denmark,Norway na Finland...ambapo kwasasa yuko chimbo kujiandaa vyema kwa ziara hiyo ambayo kwa hakika itakuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wabongo waishio ktk nchi zilizotajwa hapo juu.

Ziara hili limekuja baada mafanikio ya ziara yake ya mwaka jana nchini Uholanzi.

Haya kaka mungu akupe nini....nenda kafanye kweli...sio ukalete misifa tena huko!

JITA RECORD'S SASA YAWA TISHIO DAR


Jita Record's sasa inazidi umiza vichwa baadhi ya wa miliki wa studio kutokana na ubora wa kazi zinazo fanyika hapo pia producer XG a.k.a GOD nyani anazidi umiza pia vichwa vya ma producer wengine baada ya kukamirisha kazi ya msanii mahiri wa mziki wa Hiphop Mansuli