Friday, April 4, 2008

BSS wakamatishwa Bingo zao!



Mshindi wa (BSS) Bongo Star Search 2008,mwanadada Misoji Mkwabi jana alikamatishwa rasmi zawadi zake za ushindi kutoka kwa wadhamimi wa shindano hilo.

Mbali na mwanadada huyo wengine waliokabidhiwa zawadi zao...ni wale washiriki wengine waliobahatika kufikia hatua ya top 10.

Zawadi zilizotolewa kwa mshindi wa kwanza ni hundi ya dola za kimarekani 15,000,Television inchi 29 kutoka Kampuni ya LG, simu ya mkononi, fulana, kutoka kampuni hiyo hiyo, seti ya Sofa, kutoka Kampuni ya Living Room, Computer....pamoja na kurekodi albamu katika studio ya GMC.
Mbali na zawadi hiyo pia Misoji alikabidhiwa zawadi ya Sh. milioni 1 taslimu kutoka (FHI) Family Health Internation, kwa ajili ya kutunga nyimbo bora ya Ukimwi.

Mshindi wa pili katika shindano hilo, ambaye ni Rogers Lucas alizawadiwa Fridge,Simu ya mkononi, kutoka Kampuni ya LG,Computer....Sh. 500,000 kutoka Benchmark, pamoja na zawadi ya nguo kutoka kwa moja ya wadhamini Mariedo Botique na Sh. 150,000 kutoka FHI kwa ajili ya kutunga nyimbo ya Ukimwi.

Mshindi wa tatu katika shindano hilo, ambaye ni Elynema Mbwambo alizawadiwa DVD player, simu ya mkononi, kutoka Kampuni ya LG, Komputa kutoka Desktop, Sh. 500,000, kutoka Benchmark, nguo kutoka Mariedo Botique, pamoja na hundi ya Sh. 500,000 kutoka Shear Illusion.

Wakati mshindi wa nne katika shindano hilo ni Yohana Simon, aliyezawadiwa pesa taslimu Sh. 500,000 kutoka Benchmark, Min Stereo, simu ya mkononi kutoka LG, komputa kutoka Desk top, pamoja na mavazi kutoka kwa Mariedo Botique.

Maangaza Nyange ambae alikuwa mshindi wa tano katika shindano hilo, alizawadiwa Sh. 500,000 kutoka Benchmark, Computer, kutoka Desktop,simu ya mkononi, kutoka LG, pamoja na mavazi kutoka Mariedo Botique, pamoja na sh 600,000 kwa ajili ya kuwa mshindi wa pili wa kutunga nyimbo inayohusu ukimwi.

Washiriki wengine waliongia katika 10, bora walipata kifuta jasho cha sh 500,000 kutoka Benchmark, pamoja na simu za mkononi kutoka Kampuni ya LG.

No comments: