Thursday, December 27, 2007

Hii ndo Bongo"piga kufuri kwa usalama wako"



Unaoonekana kushoto ndio mtaa wa Aggrey kuelekea Mtaa wa Msimbazi kama unatoka TBL ulivyo leo, umejaa maduka na maghorofa yanayojengwa kila siku. Baada ya miezi mitatu ijayo hapa pataonekana vingine.

Mastaa wa BBA 2007


Richard na mkewe Ricky (kulia) na Code na mkewe Juna jana mbele ya Press! PATA HABARI KAMILI HAPA: WWW.GLOBALPUBLUSHERSTZ.COM

Hawa ndo mastaa wa Move Bongo



Hawa ndio mastaa wa filamu wa Bongo waliojuu kwa sasa! Tumepewa taarifa, tayari staa mmoja wa filamu Bongo, Steve Kanumba, ametua Hollywood Marekani kwa mwaliko rasmi kutoka John Wayne International Movie Award (?)..Waughaibuni mnaifahamu hii...tupemi taarifa!

TMK FAMILY


TMK Family
Pamoja na kukumbwa na dhoruba kali, ambalo liliwafanya wagawanyike, vijana wa TMK Wanaume Family walisimama imara katika game na hatimaye watajwa kuwa kundi lililofanya vizuri mwaka huu. Pini zao kama Kazi ipo, Pisha njia, Dar Mpaka Moro, huku wakiingiza sokoni albamu tatu kwa mpigo ni ushahidi tosh

Z ANTO


Z-Anto
Msanii chipukizi aliyetajwa kufunga mwaka kwa mafanikio makubwa, hasa baada ya kuachia albamu yake yenye jina la Binti Kiziwi, huku nyimbo zake kama Mpenzi jini na huo uliobeba jina la albamu zikifunika ile mbaya

Richard Mshindi BBA 2007


Mshindi wa BBA Africa Richard Akishangilia Baada ya kutangazwa kuwa mshindi siku ya Jumapili hiyo ambapo aliibuka na kitita cha pesa.

Jokate avutia zaidi?


Napenda nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwa hai leo hii na kuendelea na kazi yangu na kwa kukuwezesha wewe kuwa katika hali nzuri kiafya ambayo imekufanya uwe na uwezo wa kusoma safu hii.
Wote tunajua kwamba tupo katika siku mbili tatu za mwisho ili tuumalize mwaka, ni kipindi kigumu, lakini tunafahamu kwamba kama sio kwa mapenzi yake muumba, tusingeweza kuzihesabu siku hizi za mwisho wa mwaka zilizobaki.

Hata hivyo, wengi wetu tunamaliza mwaka huku tukiwa na machungu tele moyoni kutokana na kutenda na wale tuliowapenda na kuwathamini hivyo kwa kutambua hili nimeamua kuwakumbusha dada zangu mambo ambayo yanaweza kuwatoa katika mateso ya mahaba.

Boxing Day


katika kuadhimisha boxing dei leo na tumpongeze bingwa wa dunia wa kickboxing mmbongo japhet kaseba (kulia) kwa kuchaguliwa kuwa mwanamichezo bora wa mwezi Novemba mwaka huu.
kaseba alichaguliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo tanzania (taswa) kwa kura 160 mbele ya grace daudi, mfungaji bora wa mpira wa kikapu katika mashindano ya Kombe la Nje ambaye aliyepata kura 132 na catherine mapuwa wa ngome, pia mpira wa kikapu, ambaye alipata kura 104.

wachezaji waliopata kuwa wanamichezo bora wa mwezi kwa kufanya vizuri toka januari mwaka huu ni haruna moshi (soka) masoud Amour (judo), banuelia mrashani ( riadha), ali mustapha ' Barthez; (soka), joseph dimei (riadha), erasto nyoni ( soka), martin sule (riadha), kudra omar ( soka) , osward Morris ( soka) na Mary Meshack (kikapu).

Rais Kikwete


Tarehe 21/12/2007 ilitimia miaka miwili kamili tangu Rais Kikwete aapishwe kuwa Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika kuzingatia miaka hiyo miwili Rais Kikwete alikutana na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ambapo alifanya mahojiano nayo.
Ifuatayo ni sehemu ya mwanzo tu wa mahojiano hayo. Unaweza kuyasikiliza mahojiano hayo kwenye tovuti yetu mpya ya http://www.klhnews.com eneo la Podcasts.
Title: KLH News Episode: Mahojiano ya waandishi na Rais Kikwete
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2007-12-25T22_31_31-08_00
Enjoy!

WAKALI KWANZA


Hiki ni kichwa kigeni kabisa kutoka 'Wakali Kwanza' kilichovumbuliwa na kundi la Wakali Kwanza, anafahamika kama Nimo na wimbo 'Vumilia' ndio umemtambulisha rasmi kwenye ramani ya muziki nchini.

Msanii huyu alianza kuimba tokea alipokuwa anasoma huko nchini Malawi na baada ya kumaliza masomo yake alirudi nchini mwaka 2006 na kujiunga na kundi la Wakali Kwanza ila hakuweza kutoka hapo mwaka jana kutokana na shughuli binafsi zilizokuwa zinamkabili.

"Nilikuwa napenda sana kuimba, na nakumbuka kipindi nilipokuwa nasoma nilikuwa natumia muda wangu mwingi kuimba na niliamini siku moja nitakuja kuwa mkali kama..........

OKOA HIPHOP NI SO!!


Bongo5 issue namba 3 is out and Adili na nduguze wa kwenye OKOA Hip Hop wakiwa kwenye Front page.

CPWAA


Simuyangukamera captured a moment na mmoja ya actor na msanii maarufu wa michezo ya kwenye ya Luninga,KANUMBA.Very soon mtasikia CPWAAA nimeingia kwenye FILM INDUSTRY,stay tuned

HAFSA NYOTA ILIYO NG'ARA 2007


Leo HAFSA KAZINJA a.k.a PRESHA came to pressurized the building.Hafsa ametikisa mwaka huu na singo yake ya Presha aliyomshirikisha Banana zorro.Kwa mujibu wa KACHUMBARIFLAVA moja ya brand za Push Mobile hii hapa ni list ya Top selling ringtones(milio ya simu) in Tanzania 2007

J4 BSS 2007


Lile zoezi la kumtafuta star wa bongo mwenye kipaji cha muziki BONGO STAR SEARCH limeamua kuanzisha na jarida lake kabisa ambalo sasa linapatikana mitaani likishehena habari na matukio yote ikiwemo majaji na washiriki.vile vile wapo na official website yao ya BONGOSTARS.COM kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Banana


Biashara ya majarida imeshamiri sana siku hizi.Hapo juu ni new issue ya jarida la Excel ambapo front page Banana zoro ameuza na mpenzi wake Suzy ambaye ni Mke mtarajiwa.

kikwete Rais wa Tanzania Shupavu



Leo ni miaka miwili tangu Rais Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani. Mambo mengi yamefanyika katika kipindi hiki cha miaka miwili, yapo yanayo kubalika na ambayo hayakubaliki na wachache. Pia leo gazeti la Kiswahili la Serikali linatimiza mwaka mmoja gazeti hili ni HabariLEO- www.habarileo.co.tz gazeti hili kuanzishwa kwake ilikuwa ni moja ya sera za chama tawala kuwafikishia habari wananchi wa kawaida. Tuna yepi ya kusema wadau juu ya miaka hii miwili. Uwanja ni wetu hapa.

Maximo atimiza ndoto


Ndoto za kuuza wachezaji nje zatimia
Pamoja na kupewa lawama za kila aina kuwa hana uwezo katika mpira wa Soka, hatimaye Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Marcio Maximo ndoto zake za kuuza wachezaji nje ya nchi zimeanza kuonyesha matumaini ya kutimia.
Michuano ya chalenji ambayo iliweza kumalizika mwishoni mwa wiki iliyopita, imeweza kuwapa nafasi wachezaji baadhi wa Kilimanjaro Stars kwa kwenda kufanya majaribio barani Ulaya.

Wachezaji wa timu ya Kili Stars walionaswa katika michuano hiyo ni pamoja na Nahodha wa Kilimanjaro Stars Hanry Joseph akiwemo na Uhuru Suleiman.

Hatimaye kupatikana kwa wachezaji hao ni kutokana na juhudi za Maximo, kuweza kuipandisha Tanzania katika kiwango cha FIFA hadi kufikia nafasi ya 89
Sasa wa weza pata Habari za Masuper starz wa Bongo kupitia blog hii

Joan azidi kuwa tishio


Taa inayo ng'ara ndani ya 'Jumba la Dhahabu'
Mwana dada huyu ni msanii wa muziki na vilevile ni msanii kwa upande wa maigizo, Joan David Matovolwa ndilo jina lake halisi tangu angali mtoto mpaka sasa, baada ya kuingia katika sanaa ya muziki pamoja na sanaa ya kuigiza alianza kujulikana kwa jina lile lile lake la Joan.
Alianza kujishughulisha na masuala ya muziki wa Bongo flava mwaka 2002 yeye mwenyewe kwa kulipua singo zake yeye mwenyewe zilizokwenda kwa jina la 'Unastahili', 'Nakuita' pamoja na 'Nafsi'. Baada ya hapo alikuja kujisughulisana na sanaa ya maigizo, alianza sana hiyo mwaka 2005 mpaka kufikia hapa alipo katika tamhtilia ya Jumba la Dhahabu.

Akielezea sanaa ya bongo sanaa ya bongo alisema kwamba kwa sasa bado ni changa kwani wenzetu wa nchi nyyingine 'Mamtoni' wameanza sanaa kitambo na pia hutupita/kutuzidi kwa mambo mengi kwani waigizaji wa hapa kwetu Tanzania 'Bongo' tunatakiwa tuzidishe juhudi sana ili mafanikio yetu yaweze kuwa juu ili sanaa ya bongo iweze kuwa juu zaidi kama wenzetu wa nchi za mbali.

Joan alizaliwa miaka 27 iliyopita katika Hospitali ya wilaya Igunga mkoa wa Tabora. Mwaka 1988 alianza elimu ya Msingi yaani darasa la kwanza katika shule ya Msingi iitwayo Amani iliyopo Dododma mpaka alipohitimu darasa la saba mwaka 1994.

Aliweza kubahatika kuendelea na elimu ya sekondari mwaka 1995 kwa kuanza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Dodoma hadi mwaka 1998.

Kwa upande wqa matatizo katika sanaa kwa ujumla, alisema kwamba hakuna matatizo makubwa kwani mambo ambayo ni lazima ukumbane nayo ukiwa kama msanii kwa upande wa uigizaji au msanii wa muziki lazima ukumbane na matatizo kama vile usumbufu unaojitokeza kutoka kwa mashabiki wa muziki unaoufanya au hata kwa wapenzi wa sanaa ya maigizo unayoifanya.

Alisema akiwa kama msanii kwa upande wa maigizo na hata wa muziki, anatarajia kuja kuwa msanii bora ili hapo baadae aweze kuja kuwa juu zaidi kujulikana hata nchi za nje na pia kwa sanaa ya muziki anapenda kuja kuwa Projuza katika nchi mbalimbali hapo baadaye.

Ushauri wake katika sanaa ya maigizo anawaeleza na kuwashauri wasanii wenzake kwamba wataumbe fika sanaa ya bongo kwa upande wa kuigiza ni kazi sana kwani mtu anatakiwa awe na bidii ya kujituma, kwani atapata mafanikio kama zilivyo kazi nyingine.

Na ushauri wake wa mwisho ni kwa upande wa sanaa ya muziki, anawashauri sana wasanii wa muziki huu wa kizazi kipya 'Bongo Flava' kwa wale wasanii chipukizi wanatakiwa wajijue kuwa wanakipaji gani mpaka kuingia katika sanaa ya muziki, na kwa wale wasanii wa muziki ambao ni mastaa wasilewe sifa bali wakaze buti kwani muda si mrefu wasanii chipukizi wanaweza kuwa juu yao kimuziki.

Kwa sasa Joan anaendelea na masuala ya muziki na pia anaendelea na sanaa ya maigizo, kwani anaendelea na kuigiza katika tamthilia ya Jumba la dhahabu inayorushwa katika Televisheni ya Taifa ya TVT.

Tunaona katika tamthilia hiyo msanii huyo ameigiza kama mtoto wa Mzee tajiri na jambazi katika filamu hiyo, na pia binti huyo alitokea kumpenda kijana Basupa ambaye alikuja kutekwa na majambazi wa baba yake katika tamthilia hiyo Mzee Chilo.

Katika tamthilia hiyo Joan amezaliwa yeye pamoja na kaka yake Cojack ambaye anarithi kazi ya baba yake, Joan na Cojack wanapinga baba yao kumuoa Bi Moza ambapo siku ya kuvalishana pete ilipofika kijana Cojack aliweza kumpa baba yake Mzee Chilo mkwara wa nguvu kuwa endapo atamvalisha Bi Moza pete ya uchumba na yeye atamuuwa atamuuwa mzee kankakaa ambaye alikuwa emetekwa na baba yake lakini yeye alimtorosha.

Mr Nice akamua nyatunyatu


Mr Nice akamua nyatunyatu!
Pamoja na kufilisika kwake kunakosemwa na wengi hapa Bongo,msanii Lucas Mkenda 'Mr Nice' ameonekana kutokata tamaa na kujichanganya kila mahali kujaribu kutafuta riski.

Hayo yalithibitika mwishoni mwa wiki iliyopita...ambapo shuhuda wetu akiwa ktk anga zake za kula kinywaji maeneo ya Bagamoyo..alimfuma Mr Nice kwenye hoteli ya Paradise akiwa na Mike kubwaa mkononi akipiga show ya Live ya kukata na shoka kuburudisha wateja wa hoteli hiyo.

Akiwa haamini alichokuwa akikiona kutokana na maneno mengi kusemwa kuhusu msanii huyo,shuhuda huyo aliamua kufanya uchunguzi wa kinyatunyatu ili kujua bendi hiyo anayoimbia inaitwaje na inamilikiwa na nani.

Katika hangaikahangaika yake aliweza kumbana mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo aliyemweleza kuwa kwa anavyojua yeye bendi hiyo inamilikiwa na Mr Nice.

Kutokana na hilo meza yetu iliamua kumsaka Mr Nice kwa siku kadhaa bila mafanikio....nia yetu ikiwa ni kutaka kujua bendi hiyo ameianzisha lini na inaitwaje..na kama sio ya kwake ni ya nani!

jahffarai kuaga mwaka




Jahffarai kuaga mwaka hivii!
Tukiwa tunajiandaa kumalizia mwaka wa 2007 na kuukaribisha mwaka wa 2008,msanii Jahffarai anajiandaa kuachia singo itakayokuwa zawadi ya kufunga mwaka 2007 kwa wapenzi wote wa muziki wake.

Hayo yalithibitishwa na Jahffarai mwenyewe na kuitaja zawadi hiyo ya singo kuwa itaitwa 'Am in luv'...ambayo imetengenezwa kwenye studio za Big Time production chini ya producer makini Said Komorie.