Thursday, December 27, 2007

Mr Nice akamua nyatunyatu


Mr Nice akamua nyatunyatu!
Pamoja na kufilisika kwake kunakosemwa na wengi hapa Bongo,msanii Lucas Mkenda 'Mr Nice' ameonekana kutokata tamaa na kujichanganya kila mahali kujaribu kutafuta riski.

Hayo yalithibitika mwishoni mwa wiki iliyopita...ambapo shuhuda wetu akiwa ktk anga zake za kula kinywaji maeneo ya Bagamoyo..alimfuma Mr Nice kwenye hoteli ya Paradise akiwa na Mike kubwaa mkononi akipiga show ya Live ya kukata na shoka kuburudisha wateja wa hoteli hiyo.

Akiwa haamini alichokuwa akikiona kutokana na maneno mengi kusemwa kuhusu msanii huyo,shuhuda huyo aliamua kufanya uchunguzi wa kinyatunyatu ili kujua bendi hiyo anayoimbia inaitwaje na inamilikiwa na nani.

Katika hangaikahangaika yake aliweza kumbana mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo aliyemweleza kuwa kwa anavyojua yeye bendi hiyo inamilikiwa na Mr Nice.

Kutokana na hilo meza yetu iliamua kumsaka Mr Nice kwa siku kadhaa bila mafanikio....nia yetu ikiwa ni kutaka kujua bendi hiyo ameianzisha lini na inaitwaje..na kama sio ya kwake ni ya nani!

No comments: