Thursday, December 27, 2007

Sasa wa weza pata Habari za Masuper starz wa Bongo kupitia blog hii

Joan azidi kuwa tishio


Taa inayo ng'ara ndani ya 'Jumba la Dhahabu'
Mwana dada huyu ni msanii wa muziki na vilevile ni msanii kwa upande wa maigizo, Joan David Matovolwa ndilo jina lake halisi tangu angali mtoto mpaka sasa, baada ya kuingia katika sanaa ya muziki pamoja na sanaa ya kuigiza alianza kujulikana kwa jina lile lile lake la Joan.
Alianza kujishughulisha na masuala ya muziki wa Bongo flava mwaka 2002 yeye mwenyewe kwa kulipua singo zake yeye mwenyewe zilizokwenda kwa jina la 'Unastahili', 'Nakuita' pamoja na 'Nafsi'. Baada ya hapo alikuja kujisughulisana na sanaa ya maigizo, alianza sana hiyo mwaka 2005 mpaka kufikia hapa alipo katika tamhtilia ya Jumba la Dhahabu.

Akielezea sanaa ya bongo sanaa ya bongo alisema kwamba kwa sasa bado ni changa kwani wenzetu wa nchi nyyingine 'Mamtoni' wameanza sanaa kitambo na pia hutupita/kutuzidi kwa mambo mengi kwani waigizaji wa hapa kwetu Tanzania 'Bongo' tunatakiwa tuzidishe juhudi sana ili mafanikio yetu yaweze kuwa juu ili sanaa ya bongo iweze kuwa juu zaidi kama wenzetu wa nchi za mbali.

Joan alizaliwa miaka 27 iliyopita katika Hospitali ya wilaya Igunga mkoa wa Tabora. Mwaka 1988 alianza elimu ya Msingi yaani darasa la kwanza katika shule ya Msingi iitwayo Amani iliyopo Dododma mpaka alipohitimu darasa la saba mwaka 1994.

Aliweza kubahatika kuendelea na elimu ya sekondari mwaka 1995 kwa kuanza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Dodoma hadi mwaka 1998.

Kwa upande wqa matatizo katika sanaa kwa ujumla, alisema kwamba hakuna matatizo makubwa kwani mambo ambayo ni lazima ukumbane nayo ukiwa kama msanii kwa upande wa uigizaji au msanii wa muziki lazima ukumbane na matatizo kama vile usumbufu unaojitokeza kutoka kwa mashabiki wa muziki unaoufanya au hata kwa wapenzi wa sanaa ya maigizo unayoifanya.

Alisema akiwa kama msanii kwa upande wa maigizo na hata wa muziki, anatarajia kuja kuwa msanii bora ili hapo baadae aweze kuja kuwa juu zaidi kujulikana hata nchi za nje na pia kwa sanaa ya muziki anapenda kuja kuwa Projuza katika nchi mbalimbali hapo baadaye.

Ushauri wake katika sanaa ya maigizo anawaeleza na kuwashauri wasanii wenzake kwamba wataumbe fika sanaa ya bongo kwa upande wa kuigiza ni kazi sana kwani mtu anatakiwa awe na bidii ya kujituma, kwani atapata mafanikio kama zilivyo kazi nyingine.

Na ushauri wake wa mwisho ni kwa upande wa sanaa ya muziki, anawashauri sana wasanii wa muziki huu wa kizazi kipya 'Bongo Flava' kwa wale wasanii chipukizi wanatakiwa wajijue kuwa wanakipaji gani mpaka kuingia katika sanaa ya muziki, na kwa wale wasanii wa muziki ambao ni mastaa wasilewe sifa bali wakaze buti kwani muda si mrefu wasanii chipukizi wanaweza kuwa juu yao kimuziki.

Kwa sasa Joan anaendelea na masuala ya muziki na pia anaendelea na sanaa ya maigizo, kwani anaendelea na kuigiza katika tamthilia ya Jumba la dhahabu inayorushwa katika Televisheni ya Taifa ya TVT.

Tunaona katika tamthilia hiyo msanii huyo ameigiza kama mtoto wa Mzee tajiri na jambazi katika filamu hiyo, na pia binti huyo alitokea kumpenda kijana Basupa ambaye alikuja kutekwa na majambazi wa baba yake katika tamthilia hiyo Mzee Chilo.

Katika tamthilia hiyo Joan amezaliwa yeye pamoja na kaka yake Cojack ambaye anarithi kazi ya baba yake, Joan na Cojack wanapinga baba yao kumuoa Bi Moza ambapo siku ya kuvalishana pete ilipofika kijana Cojack aliweza kumpa baba yake Mzee Chilo mkwara wa nguvu kuwa endapo atamvalisha Bi Moza pete ya uchumba na yeye atamuuwa atamuuwa mzee kankakaa ambaye alikuwa emetekwa na baba yake lakini yeye alimtorosha.

No comments: