Thursday, December 27, 2007

Maximo atimiza ndoto


Ndoto za kuuza wachezaji nje zatimia
Pamoja na kupewa lawama za kila aina kuwa hana uwezo katika mpira wa Soka, hatimaye Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Marcio Maximo ndoto zake za kuuza wachezaji nje ya nchi zimeanza kuonyesha matumaini ya kutimia.
Michuano ya chalenji ambayo iliweza kumalizika mwishoni mwa wiki iliyopita, imeweza kuwapa nafasi wachezaji baadhi wa Kilimanjaro Stars kwa kwenda kufanya majaribio barani Ulaya.

Wachezaji wa timu ya Kili Stars walionaswa katika michuano hiyo ni pamoja na Nahodha wa Kilimanjaro Stars Hanry Joseph akiwemo na Uhuru Suleiman.

Hatimaye kupatikana kwa wachezaji hao ni kutokana na juhudi za Maximo, kuweza kuipandisha Tanzania katika kiwango cha FIFA hadi kufikia nafasi ya 89

No comments: