Tuesday, January 1, 2008

Hatimaye Banana Zorro na Suzy Walele jana walifunga pingu za maisha


Jana ndio ilikuwa jana.Kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa,Banana Zorro na Suzy Walele jana walifunga pingu za maisha.Pichani ni Banana Zorro akimlisha keki mkewe Suzy Walele.Sherehe hiyo iliyofana ilifanyika katika ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar-es-salaam.Banana na Suzy wamefungua ukurasa mpya.BC inawatakia kila la kheri.Kwa picha zaidi endelea hapa

(more…)

Mwana FA



Pichani ni Hamisi Mwinjuma aka Mwanafalsafa(MwanaFA).Msanii huyu wa muziki wa kizazi kipya ni miongoni mwa wasanii ambao wanasifika sana kwa kuwa na mashairi makali na yenye ujumbe mzito nchini Tanzania.Pengine yeye mwenyewe alilijua hilo wakati anaingia kwenye fani ya muziki na ndio maana akaamua kujiita Mwanafalsafa.Hatujui,siku moja tutamuuliza.

Mwanafalsafa ameshatunga mashairi na nyimbo nyingi.Miongoni mwa nyimbo au mashairi hayo ni lile ambalo inasemekana ndio “lilimtoa”.Aliliita “Ingekuwa Vipi”.Humo alikuwa anahoji mambo kadhaa kama vile;

Ingekuwa vipi Yesu angerudi?Angemaliza vita ya Wapalestina na Wayahudi? lngekuwa vipi kama Osama angeutawala Ulimwengu?Wamarekani Uarabuni wangekuwa Sungusungu?Ungekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini?Dunia bila dhambi,Kipimo cha uovu nini?Polisi, mahakama na gerezani angeenda nani?Vipi kama Wazungu wasingeingia Afrika? Magari, ndege, Reli na nguo, nani angeleta?Na bila biashara ya utumwa wangekuwepo black Americans? …na mengineyo.

Unaweza kuusikiliza wimbo huo wa MwanaFA kupitia EastafricanTube kwa kubonyeza hapa.