Thursday, December 27, 2007

Boxing Day


katika kuadhimisha boxing dei leo na tumpongeze bingwa wa dunia wa kickboxing mmbongo japhet kaseba (kulia) kwa kuchaguliwa kuwa mwanamichezo bora wa mwezi Novemba mwaka huu.
kaseba alichaguliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo tanzania (taswa) kwa kura 160 mbele ya grace daudi, mfungaji bora wa mpira wa kikapu katika mashindano ya Kombe la Nje ambaye aliyepata kura 132 na catherine mapuwa wa ngome, pia mpira wa kikapu, ambaye alipata kura 104.

wachezaji waliopata kuwa wanamichezo bora wa mwezi kwa kufanya vizuri toka januari mwaka huu ni haruna moshi (soka) masoud Amour (judo), banuelia mrashani ( riadha), ali mustapha ' Barthez; (soka), joseph dimei (riadha), erasto nyoni ( soka), martin sule (riadha), kudra omar ( soka) , osward Morris ( soka) na Mary Meshack (kikapu).

No comments: